Jamaa ambao wamechukua msimamo wa kunyamaza


Nilimuuliza Abu ´Abdillaah juu ya mtu ambaye baba yake amenyamaza kuhusu kuumbwa kwa Qur-aan. Akajibu:

“Amwamrishe na amfanyie upole.”

Nikamuuliza akiacha kuzungumza naye ikiwa atashikilia maoni yake. Akajibu:

“Ndio.”

Nikamuuliza Abu ´Abdillaah juu ya mtu ambaye dada yake au shangazi yake ameolewa na mtu ambaye amenyamaza juu ya uumbwaji wa Qur-aan. Akajibu:

“Akutane naye na amsalimie.”

Nikamuuliza ikiwa ni nyumba ya mwanamme huyo ambapo akajibu:

“Asimame nje ya mlango na asiingie ndani.”

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Abiy Harb al-Jarjaara’iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Masaa-il-ul-Imaam Ahmad, uk. 13-14
  • Imechapishwa: 13/03/2021