Swali: Je, Mtume ´Iysaa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) atakufa baada ya kushuka ardhini au yeye hatokufa?

Jibu: Bali atakufa. Hakuna mtu yeyote ambaye hatokufa. Amesema (Ta´ala):

كُلُّ نَفْسٍ ذَائِقَةُ الْمَوْتِ

“Kila nafsi itaonja kifo.” (03:185)

Neno lake ´kila` limejumuisha nafsi zote akiwemo ´Iysaa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kwani na yeye ni nafsi miongoni mwa nafsi. Imekuja vilevile katika Hadiyth ya kwamba baada ya kuhukumu kwa Shari´ah ya Mtume wetu (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) basi atakaa kwa muda fulani. Imekuja vilevile katika baadhi ya Hadiyth zengine kwamba atakaa siku saba halafu baada ya hapo atakufa kifo alichoandikiwa na Allaah na kuzikwa ndani ya ardhi kama wengine. Hakuna kitachobaki isipokuwa uso wa Allaah.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (09) http://audio.islamweb.net/audio/index.php?page=FullContent&audioid=191370#219699
  • Imechapishwa: 06/03/2019