Istihzai chache inayomfanya mtu kukufuru

Swali: Ni istihzai ipi chache ambayo inamfanya yule mwenye kufanya hivo kukufuru?

Jibu: Haina uchache. Ni mamoja iwe kubwa au ndogo. Haina uchache. Kila aina ya istihzai na maskhara – wanachuoni wamesema hata kufanya ishara kwa macho, midomo, mikono – kunaingia katika istihzai. Haijalishi kitu hata kama mtu hakuongea.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam, uk. 140
  • Imechapishwa: 23/12/2018