ISIS Ni Wabaya Zaidi Kuliko Khawaarij Wa Kale

(Khawaarij) wana khatari kubwa leo kwa sababu baadhi ya watu wamedanganyika nao. Kwa sababu wanasema kila wakati Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wamesema pasina kutendea kazi wayasemayo. Wanachofanya ni kuyagonganisha maandiko, kama alivyosema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallan). Wanasoma Qur-aan pasi na kuvuka koo zao. Kwa ajili hiyo ndio maana tunatakiwa kutahadhari nao na wale wenye kulingania kwao, kuwapa udhuru au mwenye kuwaonea huruma.

Wale wanaohalalisha damu za waislamu kama ISIS – lau ungelijua ni kina nani ISIS – na wale wenye mfumo wao ni wabaya zaidi kuliko Khawaarij wa kale. Khawaarij wa kale walikuwa wa wazi. Hawa wa leo hawako wa wazi na wanaenda kwa kanuni inayosema “lengo zuri linahalalisha njia”. Wanahalalisha mambo ya haramu ambayo Khawaarij wa kale walikuwa wanayachukulia kuwa ni kufuru. Kwa ajili hii naonelea kuwa ni watenda dhambi wakubwa kuliko Khawaarij wa kale. Haijalishi kitu sawa ikiwa wataitwa “al-Qaa´idah”, “ISIS” au kitu kingine.

Kosa kubwa ni kuona miji ya kikafiri na wengine ambao ndio wameunda watu hawa wanawaita kuwa ni “nchi ya Kiislamu”. Hili ni kosa. Sisi hatuwatambui kuwa ni nchi ya Kiislamu. Ingelikuwa bora kuwaita kama jinsi wao wenyewe mwanzoni walivyokuwa wanajiita “ISIS” tu. Ama kuwaita kuwa ni “nchi ya Kiislamu” hii ni dhuluma, uongo, batili na uadui. Wametoka kwa waislamu. Wameua maelfu ya waislamu. Wanashirikiana bega kwa bega na shetani wa Syria na wengine kuwaua waislamu.

Mambo yanahusiana na dini na kuwa na uelewa juu ya dini ya Allaah (´Azza wa Jall). Dini ya Allaah (´Azza wa Jall) inachukuliwa kutoka kwa wanachuoni Rabbaaniyyuun ambao wanarudisha upotoshaji wa wavuka mipaka, madai ya watu wa batili na tafsiri za wajinga. Dini haichukuliwi kutoka kwenye makopo ya takataka za Intaneti. Tunasoma kwa Intaneti kisha tunajiunga na kundi hili la wakataji na lililopinda?

Kuweni makini na wavulana na wasichana zenu! Wekeni macho yote kwenye vifaa hivi wanavyozunguka navyo. Ima wanaeneza tovuti za ngono na mambo mengine yenye kuita katika ngono, ujuvi na kufanya uasi dhidi ya dini ya Allaah au wanaeneza madhehebu ya Khawaarij ambao wamejipenyeza katika dini ya Allaah (´Azza wa Jall).

  • Mhusika: Shaykh Swaalih bin Sa´d as-Suhaymiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.sahab.net/forums/index.php?showtopic=150993 1436-05-17/2015-03-08
  • Imechapishwa: 06/11/2016