Inatosha kumwaga maji juu ya mgongo wakati wa kuoga janaba

Swali: Mgongoni mwangu kuna sehemu kiasi cha shibiri ambapo mkono wangu haufiki ili niweze kupaosha. Je, nifanya Tayammum wakati wa kuoga janaba?

Jibu: Ikiwa huwezi kupangusa basi unaweza kupamwagia maji sehemu hii na inatosha. Midhali utapamwagia maji kama vile unavyomwagia mgongoni kawaida, hilo linatosha.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (54) http://binothaimeen.net/content/1222
  • Imechapishwa: 04/09/2019