Inatosha Ibn Baaz na Ibn Humayd kuwa wanafunzi wake

Swali: Tumesikia mara nyingi kuhusu wanachuoni kama mfano wa Imaam Muhammad bin Ibraahiym (Rahimahu Allaah). Unaweza kutueleza kitu juu yake khaswa ukizingatia kwamba wewe pia ulikuwa mwanafunzi wake?

Jibu: Shaykh Muhammad bin Ibraahiym (Rahimahu Allaah) alikuwa ni imamu mtukufu. Inatosha kuwathibitishieni kwamba miongoni mwa wanafunzi zake alikuwa Imaam na Shaykh ´Abdul-´Aziyz bin Baaz na Imaam na Shaykh ´Abdullaah bin Humayd. Inatosha kwamba maimamu hawa ni miongoni mwa wanafunzi wa Shaykh Muhammad bin Ibraahiym (Rahimahu Allaah). Walisimama mahali pake baada ya kufa kwake na wakatekeleza yale yenye kuwawajibikia katika waliyoeneza katika elimu, wakasimamisha dini hii na wakaamrisha mema na kukataza maovu. Hivi sasa ni wakati wenu nyinyi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.alfawzan.af.org.sa/ar/node/18073
  • Imechapishwa: 12/07/2019