Inasihi kufunga siku tatu katika kafara ya yamini mtu akiwa na uwezo wa kulisha?

Swali: Kuna mtu aliapa juu ya kitu kisha akatimiza kiapo chake ambapo akafunga pamoja na kwamba ana uwezo wa kulisha. Ni ipi hukumu? Je, swawm inasihi pamoja na kwamba Allaah ameanza kwanza kwa kulisha na akafanya kufunga ni pale ambapo mtu atakosa cha kulisha? Je, hukumu inatofautiana ikiwa alikuwa hajui hukumu?

Jibu: Mtu akifunga katika kafara ya yamini na yeye ni muweza wa kuwalisha masikini kumi, kuwavisha au kuachia mtumwa huru, basi swawm hiyo inakuwa ni ya sunnah na ni lazima kwake kutekeleza kafara yake. Lakini hata hivyo swawm yake haipotei na inakuwa ni ya sunnah kwake. Anatakiwa alishe.

Ni jambo limeenea kwa watu wengi kwamba kafara ya yamini ni kufunga. Kwa ajili hii akimuapia nduguye kwamba atafanya jambo fulani utamuona anamwambia kwamba usinifanye nikafunga siku tatu. Hili ni kosa. Kulisha ndio kunatangulizwa kwanza, kuvisha au kuacha mtumwa huru. Asipopata mambo haya ndio anatakiwa kufunga siku tatu mfululizo.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (70) http://binothaimeen.net/content/1572
  • Imechapishwa: 08/03/2020