Swali: Baadhi ya watu wanafunga na hawaswali. Je, wapewe Zakaat-ul-Fitwr?

Jibu: Wanaofunga pasi na kuswali hawana funga yoyote. Matendo yao yote ni batili. Wasioswali ni lazima kwao kutubu kwa Allaah. Wakitubu kwa Allaah na wakasilimu ndio watakuwa wameingia katika Uislamu upya na hapo ndipo wanaweza kupewa Zakaat-ul-Fitwr, wanaweza kufunga na kufanya matendo ya wajibu mengine.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/node/4846
  • Imechapishwa: 21/06/2017