Inajuzu kufuta kwenye khofu na soksi nyembamba na zilizochanika?

Swali: Kuna baadhi ya wanachuoni wenye kuonelea kuwa inajuzu kufuta juu ya kila kitu chenye kuvaliwa mguuni.

Jibu: Maoni haya anayoashiria muulizaji ambayo ni kujuzu kufuta juu ya kila kinachovaliwa mguuni ndio maoni sahihi. Hayo ni kwa sababu maandiko yaliyothibiti juu ya kupangusa kwenye khofu yameachiliwa na hayakufungamanishwa na masharti. Yaliyopokelewa kutoka katika Shari´ah kwa kuachiliwa haijuzu kuyawekea masharti. Kwa sababu kuyawekea masharti itakuwa ni kuyafunga mambo ambayo Allaah na Mtume wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wameyafanya kuwa mapana. Msingi ni kubaki kilichoachiliwa kama kilivyo na kilichoenea kama kilivyo mpaka kupokelewe dalili juu ya kukifungamanisha na kukifanya maalum.

Baadhi ya wafuasi wa ash-Shaafi´iy wamesimulia kutoka kwa ´Umar na ´Aliy bin Abiy Twaalib (Radhiya Allaahu ´anhum) kujuzu kupangusa juu ya khofu nyembamba. Hii inafahamisha kujuzu kufuta kwenye khofu na soksi nyembamba na zilizochanika.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (11/166-167)
  • Imechapishwa: 02/07/2017