Inafaa kusoma ndani ya msahafu katika Tarawiyh?

Swali: Inasihi kusoma kutoka ndani ya msahafu katika swalah ya Tarawiyh?

Jibu: Ambaye hawezi kusoma kutoka kichwani hakuna neno akasoma kutoka ndani ya msahafu katika swalah ya Tarawiyh. Kwa kuwa atasoma Qur-aan yote kuanzia mwanzo wake mpaka mwisho wake. Asome kutoka kwenye msahafu akiwa sio mwenye kuhifadhi Qur-aan. Baadhi ya Salaf walikuwa wakifanya hivi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaam al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/node/14891
  • Imechapishwa: 31/05/2017