Inafaa kusoma du´aa ya kukhitimu Qur-aan ndani ya swalah?


Swali: Baadhi ya watu wanawakemea maimamu wa misikiti ambao wanasoma du´aa ya kukhitimu Qur-aan mwishoni wa mwezi wa Ramadhaan na wanasema kwamba ni jambo halikuthibiti kutoka kwa yeyote katika Salaf. Ni upi usahihi juu ya hilo?

Jibu: Hakuna ubaya kufanya hivo. Kwa sababu imethibiti kutoka kwa baadhi ya Salaf kwamba walifanya hivo. Jengine ni kwa sababu ni du´aa ambayo kumepatikana sababu yake katika swalah. Hivyo inaingia katika jumla ya du´aa za ndani ya swalah kama vile kukunuti katika Witr na wakati wa majanga.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (30/32)
  • Imechapishwa: 21/05/2018