Inafaa kupatana juu ya pesa kwa ajili ya kuepuka adhabu?

Swali: Kuhusu ukiukaji wa heshima za watu. Je, inafaa kupatanisha kwa njia ya kutoa kiwango fulani cha pesa? Kwa mfano mtu akimshambulia mvulana kwa kumfanyia liwati au mfano wa kitu kama hicho. Wakati wa kuhukumiana kwa hakimu akamsamehe kwa kutoa kiwango fulani cha pesa. Je, inafaa?

Jibu: Hapana, haifai. Akishaingia ndani ya adhabu haifai. Kukishathibiti adhabu basi ni lazima asimamishiwe adhabu kwa mujibu wa Shari´ah. Haijuzu kupatanisha juu ya adhabu. Ni lazima asimamishiwe adhabu kwa mujibu wa Shari´ah. Isipokuwa ikiwa kama mtu atajitolea kumsitiri pasi na fidia basi atafanya hivo baada ya kutubia. Kulifisha jambo kunaingia katika kulisitiri na yule atakayemsitiri muislamu basi Allaah atamsitiri duniani na Aakhirah na hatomfichua. Katika hali hiyo hakuna neon. Lakini yafanyike pasi na fidia.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaad-ud-Duruus https://binbaz.org.sa/fatwas/6188/%D9%87%D9%84-%D9%8A%D8%AC%D9%88%D8%B2-%D8%A7%D9%84%D8%AA%D8%B5%D8%A7%D9%84%D8%AD-%D8%B9%D9%84%D9%89-%D9%85%D8%A7%D9%84-%D9%84%D8%A7%D8%B3%D9%82%D8%A7%D8%B7-%D8%A7%D9%84%D8%AD%D8%AF
  • Imechapishwa: 06/12/2020