Swali: Mtu akivaa soksi pasi na haja au kwa ajili tu ya kujipamba inafaa kwake kupangusa juu yake au ni lazima kuzivua na kupangusa juu yake?

Jibu: Uwazi wa dalili zinaonyesha kuwa mtu akivaa soksi basi inafaa kwake kufuta juu yake. Ni mamoja malengo yake iwe ni kuulinda mguu wake kutokamana na baridi, mguuni mwake kuna unyevu na akakusudia kujilinda na vumbi au akawa na malengo mengine. Ni sawa akapangusa juu yake. Lakini kupangusa kunatakiwa kuwe kwa ule muda uliowekwa katika Shar´ah. Kwa mkazi ni mchana mmoja na usiku wake na kwa msafiri ni michana mitatu na nyusiku zake. Mtu anaanza kuhesabu katika ule upangusaji wake wa kwanza baada ya kupatwa na hadathi. Ni lazima vilevile awe na wudhuu´.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (32) http://binothaimeen.net/content/727
  • Imechapishwa: 26/11/2017