Swali: Vipi mtu kuitwa jina la ´Abdus-Sayyid?

Jibu: Kuliacha ni bora zaidi kwa sababu linatatiza. Vinginevyo Sayyid (Bwana) ni katika majina ya Allaah. Kuitwa majina ya Allaah ambayo yako wazi kama mfano wa ´Abdur-Rahmaan, ´Abdul-´Aziyz, ´Abdul-Saamiy´ na ´Abdul-´Aliym ndio bora zaidi. Vinginevyo jina Sayyid halina neno, ni kama alivosema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Bwana ni Allaah (Tabaarak wa Ta´ala).”[1]

[1] Ma´rifat-us-Swahaabah (20/404) ya Abu Na´iym al-Aswbahaaniy.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat (01)
  • Imechapishwa: 22/02/2019