Swali: Atakayerudisha khabari miongoni mwa khabari za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika mlango wa mambo ya ´Aqiydah kwa kujengea kwamba ni mapokezi yaliyopokelewa kupitia Swahabah mmoja – je, huko kunazingatiwa ni kuritadi kutoka katika Uislamu?

Jibu: Akijua kuwa imesihi kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na akatambua kuwa ni dalili ya wazi katika maudhui fulani na kwamba hakuna uwezekano mwingine, ndio, kunazingatiwa ni kuritadi kwa sababu hana udhuru wowote.

Lakini ikiwa hakujua usahihi wake na kuthibiti kwake kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) au  ametambua usahihi na kuthibiti kwake, lakini Hadiyth ikawa ina uwezeno mwingine na sio dalili ya wazi katika maudhui fulani, huyu anapewa udhuru kwa sababu ya hizo wezekano zengine na kufahamu kwake kimakosa.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam, uk. 124
  • Imechapishwa: 24/11/2018