Swali: Allaah amesema:

وَمَا يُؤْمِنُ أَكْثَرُهُم بِاللَّـهِ إِلَّا وَهُم مُّشْرِكُونَ

”Wengi kati yao hawamwamini Allaah isipokuwa wao ni wenye kufanya shirki.”[1]

Ni ipi maana ya Aayah? Ni yepi makusudio ya washirikina katika Aayah hii?

Jibu: Wanazuoni, kama vile Ibn ´Abbaas na wengineo, wameweka wazi maana yake. Wamesema kuwa maana yake ni kwamba washirikina wanapoulizwa ni nani ameumba mbingu na wao wenyewe basi watasema kuwa ni Allaah. Licha ya haya wanaabudia masanamu na mizimu kukiwemo al-Laat, al-´Uzzaa na wengineo. Aidha wanayaomba uokozi, wanayawekea nadhiri na kuyachinjia. Imani yao hii ni Tawhiyd-ur-Rubuubiyyah na inaharibika kwa kule kumshirikisha kwao Allaah (Ta´ala) na wala haiwanufaishi kitu. Abu Jahl na wengineo mfano wao wanaamimi kuwa Allaah ndiye Muumbaji wao, Mruzuku wao na Muumbaji wa mbingu na ardhi. Lakini imani hii haikuwafaa kitu kwa sababu wameshirikisha kwa kuabudu masanamu na mizimu. Hii ndio maana ya Aayah kwa mujibu wa wanazuoni.

[1] 12:106

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (08/292)
  • Imechapishwa: 14/06/2021