Imamu anakula vitunguu saumu na kuja kuswalisha watu msikitini

Swali: Mimi ni imamu wa msikiti siku zote na nala kitunguu saumu na siwezi kukikosa hata siku moja pamoja na kuzingatia ya kwamba ninapokula kitunguu saumu siikai msikitini kabisa ili nisije kuwaudhi wengine. Pale ninapoingia mlango wa msikiti naenda moja kwa moja mpaka kwenye Mihraab na ninapotoka hapo naenda nje ya msikiti. Kisha naswali Sunnah nyumbani. Je, inajuzu kwangu kufanya hivo? Ni ipi njia ambayo ni bora kuliko hii?

Jibu: Haijuzu kwa mtu anapokula kitunguu maji au kitunguu saumu na kukabaki harufu kuingia msikitini. Si kwenye Mihraab, katikati ya msikiti, si imamu wala maamuma wala anayeswali peke yake. Kutokana na maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Mwenye kula kitunguu maji au kitunguu saumu basi asiikaribie misikiti yetu. Kwani hakika Malaika wanaudhika kwa yale yanayomuudhi mwanaadamu.”

Lakini ikiwa hana budi kuvila basi atumie vitu vinavyoondosha harufu ya vitunguu hivyo. Harufu ikiondoka ni sawa akahudhuria msikitini na akawa imamu, maamuma au kuswali peke yake. Lakini midhali harufu bado ni yenye kubaki haifai kwake kuingia msikitini.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (42) http://binothaimeen.net/content/941
  • Imechapishwa: 07/12/2018


Takwimu
  • 321
  • 373
  • 1,819,089