Swali: Ni ipi hukumu ya mwanamke kupunguza nywele zake?

Jibu: Ikiwa ni upunguzaji unaofikia katika kiwango cha kujifananisha na kichwa cha mwanaume ni haramu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema Allaah amewalaani wanawake wenye kujifananisha na wanaume. Vivyo hivyo ikiwa ni upunguzaji wa kujifananisha na vichwa vya wanawake wa kikafiri ni haramu vilevile. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mwenye kujifananisha na watu basi yeye ni katika wao.”

Mbali na hali hizo mbili kuna wanachuoni ambao wameharamisha kitendo hicho, kama [sauti haiko wazi] mfuasi wa Imaam Ahmad (Rahimahu Allaah), wengine wameonelea kuwa linachukiza – na ndio maoni yaliyotangaa katika madhehebu ya Imaam Ahmad – na kuna walioruhusu hilo.

Lililo salama zaidi ni mwanamke asipunguze isipokuwa wakati wa hajj au ´umrah.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (23)
  • Imechapishwa: 08/01/2019