Ibn ´Uthaymiyn kuhusu ndoa ya mwanamke aliyelazimishwa

Swali: Je, walii anaweza kumlazimisha msichana wake kuolewa?

Jibu: Hapana. Walii hana haki hiyo, sawa awe ni baba au mtu mwingine, kumlazimisha msichana wake kuolewa. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Bikira asiozeshwe mpaka atakwe kwanza idhini na wala asiozeshwe mwanamke mpaka kwanza atakwe ushauri.”

Katika upokezi wa Muslim imekuja:

“Bikira hutakwa ushauri na baba yake.”

Kwa hiyo haijuzu kwa baba kumuozesha msichana wake, dada yake wala mwanamke yeyote yule anayemsimamia mpaka kwanza aridhie. Akimlazimisha ndoa sio sashihi. Hivyo itakuwa si halali kwa mume kumwingilia kwa sababu amelazimishwa nae na kwa ajili hiyo ndoa sio sahihi.

Swali: Je, ana haki ya kuvunja ndoa?

Jibu: Tukisema kuwa ndoa sio sahihi itakuwa ni lazima kuivunja kwa kuwa haikusihi. Lakini tukikadiria kuwa mwanamke atamwendea mwanaume na kumjuzishia mwanaume ndoa mwanaume huyo, ndoa ni sahihi. Kujengea juu ya kujuzisha kwake ndoa itakuwa sahihi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (12)
  • Imechapishwa: 13/08/2017