Ibn ´Uthaymiyn kuhusu mtu kupeana kiungo chake wakati yuko hai na baada ya kufa

Haijuzu mpaka kwa aliyehai kupeana viungo vyake. Kwa mfano mvulana wako, baba yako, kaka yako au dada yako atahitajia figo basi haitofaa kumpa fijo lako. Ni haramu kwako kwa sababu zifuatazo:

1- Figo hili ambalo umetolewa wewe akapewa yeye huenda likafanyakazi kama ambavo vilevile huenda lisifanyekazi. Hata kama madaktari watakuwa na dhana yenye nguvu kwamba litafanyakazi bado kuna uwezekano lisifanyekazi. Katika hali hii utakuwa umefanya makosa ya kulitoa figo hili sehemu yake lilipowekwa na Allaah na kupelekwa sehemu ambayo huenda likafanyakazi kama ambavo vilevile huenda lisifanyekazi. Madaktari watapokuwa na dhana yenye nguvu kwamba litafanyakazi basi bado kuna uwezekano wa kutokufanyakazi.

2- Je, wewe una uhakika kuwa hilo figo lingine lililobaki litaendelea kufanyakazi salama mpaka utapokufa? Hapana. Huenda hilo figo lingine likapatwa na maradhi na hivyo wewe ukawa ndiye sababu ya kujiua mwenyewe. Kujengea juu ya hilo haijuzu kabisa kwa mtu akajitolea figo lake na wala kiugo chochote. Ni mamoja mtu bado yuko hai au amekwishakufa.

Mtu anaweza kuuliza kuhusu damu. Tulisema kuwa ni sawa mtu akajitolea damu wakati wa haja. Kwa sharti yule mwenye kujitolea asipatwe na maradhi. Tofauti kati ya damu na kiungo ni kwamba damu itakuja badala yake nyingine. Ama kiungo hakuji badala yake kingine.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (50) http://binothaimeen.net/content/1144
  • Imechapishwa: 18/06/2019