Hakuna, si katika Qur-aan wala Sunnah, yanayohalalisha makundi na vyamavyama. Bali yaliyomo kwenye Qur-aan na Sunnah ni kusemwa vibaya kwa jambo hilo. Amesema (Ta´ala):

فَتَقَطَّعُوا أَمْرَهُم بَيْنَهُمْ زُبُرًا ۖ كُلُّ حِزْبٍ بِمَا لَدَيْهِمْ فَرِحُونَ

”Lakini wakalivunja jambo lao baina yao makundi mbalimbali, kila kundi kwa waliyokuwa nayo linafurahia.”[1]

Hapana shaka kwamba vyamavyama hivi vinapingana na yale aliyoamrisha Allaah. Bali yale aliyosisitiza pindi aliposema (Ta´ala):

إِنَّ هَـٰذِهِ أُمَّتُكُمْ أُمَّةً وَاحِدَةً وَأَنَا رَبُّكُمْ فَاعْبُدُونِ

“Hakika huu ummah wenu ni ummah mmoja; Nami ni Mola wenu, hivyo basi niabuduni.”[2]

[1] 23:52-53

[2] 21:92

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa ´Ulamaa-ul-Kibaar fiy al-Irhaab wat-Tadmiyr, uk. 408
  • Imechapishwa: 18/01/2020