Ibn ´Uthaymiyn idhini ya mwanamke kukubali kuolewa

Swali: Je, ni sharti kupatikane ushahidi kwamba mke karidhia kuolewa?

Jibu: Wanachuoni wametofautiana. Madhehebu [ya Hanaabilah] yanasema kuwa imependekezwa na sio wajibu. Lakini kutokana na yale yanayoendelea hii leo katika magomvi na mfano wake tunaona kuwa ni lazima mashahidi watoe ushahidi kwamba mke amekubali.

Swali: Je, idhini yake watu wasikilizishwe?

Jibu: Idhini yake namaanisha kukubali kwake. Lakini baadhi ya wanawake ikiwa dada yake ambaye anataka kuolewa hajui kuandika wanamletea ambaye anajua kuandika na anaandika jina la dada yake [mwolewaji] na anampigia saini. Kitendo hichi ni haramu na hakifai. Bali lililo la wajibu ni mke ahudhurie, hata kama hajui kuandika, ichukuliwe idhini yake na kutosheke kwa kufanya hivo.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (76) http://binothaimeen.net/content/1755
  • Imechapishwa: 05/09/2020