Ibn ´Uthaymiyn anayestahiki na asiyestahiki kuuziwa TV   

Swali: Kuna mtu amenipa TV na ameniwekea uzito nimuuzie na iko kwangu hivi sasa na sijui nifanye kitu gani – je, niiuze na endapo nitafanya hivo nitakuwa mwenye kupata dhambi? Je, thamani yake ni haramu?

Jibu: Namzungumzisha muuliza ifuatavyo: akiuza hichi alichopewa kumuuliza mtu ambaye atakitumia kwa njia inayoruhusiwa, kwa mfano akawauzia wale wanaotazama filamu zinazowanufaisha watu haina neno. Anapata dhambi ikiwa atawauzia watu wasiokuwa wasomi. Kwa kuwa watu wengi wanazitumia hizi TV kwa mambo ya haramu. Ni jambo lisilokuwa na shaka ya kwamba kinachoangaliwa kwenye TV kuna kinachoruhusiwa, kuna kinachonufaisha na kuna kilicho cha haramu na madhara. Watu wengi hawatofautishi kati ya hayo mawili.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (02)
  • Imechapishwa: 01/05/2020