Ibn Baaz swalah ya mkusanyiko ya pili msikitini

Swali: Ikimalizika swalah na kukaja kundi la watu wengine ambao wote hawajaswali. Je, wasimamishe swalah ya mkusanyiko nyingine au kila mmoja aswali kivyake? Wapo baadhi ya wanachuoni wanaochukia kusimamisha swalah ya mkusanyiko nyingine. Tunaomba kuwekewa wazi.

Jibu: Ni lazima kwao kuswali mkusanyiko na kila mmoja asiswali kivyake. Yaliyosemwa na baadhi ya wanachuoni kwamba kila mmoja aswali kivyake ni kosa na si usawa. Lililo la wajibu waswali mkusanyiko kama ambavo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alivyoamrisha kwa yule ambaye aliingia akakuta watu wamekwishaswali akasema:

”Ni nani atakayemtendea wema huyu akaswali pamoja naye”?

Mpaka izingatiwe ni mkusaniyko. Zipo vilevile dalili zengine zinazojulisha ulazima wa mkusanyiko na fadhilah zake.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3704/ما-حكم-اقامة-الجماعة-الثانية-بالمسجد
  • Imechapishwa: 18/04/2020