Swali: Je, muheshimiwa una madhehebu maalum na ni upi mfumo wako katika fatwa na dalili?

Jibu: Madhehebu yangu katika Fiqh ni madhehebu ya Imaam Ahmad bin Hanbal (Rahimahu Allaah). Sio kwa njia ya kufuata kichwa mchunga. Ni kwa njia ya kufuata katika misingi aliyokuwa akifuata.

Kuhusu masuala ya khilafu mfumo wangu ni kuyapa nguvu yale yanayopelekea kuyapa nguvu na fatwa natoa kwa mfumo huo. Ni mamoja hilo limeafikiana au linaenda kinyume na madhehebu ya Hanaabilah. Haki ndio yenye haki zaidi ya kufuatwa. Allaah (´Azza wa Jall) amesema:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا أَطِيعُوا اللَّـهَ وَأَطِيعُوا الرَّسُولَ وَأُولِي الْأَمْرِ مِنكُمْ ۖفَإِن تَنَازَعْتُمْ فِي شَيْءٍ فَرُدُّوهُ إِلَى اللَّـهِ وَالرَّسُولِ إِن كُنتُمْ تُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ ۚ ذَٰلِكَ خَيْرٌ وَأَحْسَنُ تَأْوِيلًا

“Enyi walioamini! Mtiini Allaah na mtiini Mtume na wenye madaraka katika nyinyi. Mkizozana katika jambo basi lirudisheni kwa Allaah na Mtume mkiwa mnamuamini Allaah na siku ya Mwisho – hivyo ni bora na matokeo mazuri kabisa.”[1]

[1] 04:59

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (04/166)
  • Imechapishwa: 02/07/2017