Ibn Baaz mke kupunguza nywele kwa ajili ya kumpambia mume

Swali: Je, inafaa kwa mwanamke kupunguza nywele zake au kuzibadilisha rangi kwa sababu ya kumpambia mume wake?

Jibu: Kupunguza nywele kunategemea; haifai ikiwa lengo ni kujifananisha na maadui wa Allaah. Haijuzu kujifananisha na wanawake wa kikafiri. Ama ikiwa ni kwa ajili ya kupunguza tu na kujipamba baada ya kupata ridhaa kutoka kwa mume wake hakuna neno kupunguza.

Kuhusu kuzipaka nywele rangi hakuna kizuizi midhali si rangi nyeusi. Haijuzu kuzibadilisha kwa rangi nyeusi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Zipake rangi mvi hizi na ziepushe na [rangi] nyeusi.”

Makatazo ya kupaka rangi nyeusi ndio jambo lililotangaa kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kuhusu rangi nyingine kama nyekundu na ya manjano hakuna ubaya.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa-ud-Duruus https://binbaz.org.sa/fatwas/4633/%D8%AD%D9%83%D9%85-%D9%82%D8%B5-%D8%A7%D9%84%D9%85%D8%B1%D8%A7%D8%A9-%D9%84%D8%B4%D8%B9%D8%B1%D9%87%D8%A7-%D9%88%D8%B5%D8%A8%D8%BA%D9%87
  • Imechapishwa: 27/09/2020