Ibn Baaz kuthibiti na kuisha kwa Ramadhaan II


Swali: Ni mashahidi wangapi wanatosha juu ya kuonekana mwezi wa Shawwaal? Akiuona mtu mmoja na akajinyamazia analazimika kula au kufunga?

Jibu: Ni lazima wapatikane mashahidi wawili ambao ni waadilifu katika miezi yote mbali na kuingia kwa Ramadhaan. Kuthibiti kuingia kwake kunatosha mtu mmoja mwadilifu kwa mujibu wa maoni sahihi zaidi ya wanachuoni kutokana na yale yaliyothibiti kwa Ibn ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa):

“Watu waliona mwezi ambapo nikamweleza Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwamba mimi pia nimeuona ambapo akafunga na akaamrisha kufunga.”[1]

Ina ushahidi mzuri kupitia Hadiyth ya Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa).

Mtu akiuona mwezi peke yake na usikubaliwe ushahidi wake hatofunga peke yake na wala hakutofungua peke yake kwa mujibu wa maoni sahihi zaidi ya wanachuoni. Bali itamlazimu kwake kufunga pamoja na wengine na kufungua pamoja na wengine. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Fungeni siku mnafunga, fungueni siku mnafungua na chinjeni siku mnachinja.”[2]

[1] Abu Daawuud (2342).

[2] at-Tirmidhiy (697).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (15/64)
  • Imechapishwa: 15/05/2018