Ibn Baaz kuhusu salamu za rambirambi kwenye magazeti

Swali: Hivi karibuni jambo la rambirambi kwa wafiwa limeenea kwa kuandika kwenye magazeti. Rambirambi zinatumiwa kwa njia ya matangazo ambapo kunaandikwa jina la anayefanya hivo, jina la taasisi au kampuni. Isitoshe taazia inaweza kuendelea kwa kipidi kirefu. Unasemaje juu ya hilo? Unawanasihi nini wasimamizi wa magazeti haya?

Jibu: Sijui ubaya wa kufanya hivo. Kule kuwaandikia familia ya maiti katika gazeti kwamba wanamshukuru ambaye amewapa pole kuhusu fulani au tunampa pole fulani. Sijui ubaya wowote wa kufanya hivo. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wakati alipofariki an-Najaashiy aliwatokea watu na akawatangazia kifo chake kwamba amekufa. Baadaye akamswalia, akawaamrisha (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kumswalia. Sijui ubaya wowote wa kufanya hivo.

Kutoa mkono wa pole hakuna kikomo cha muda wa siku tatu, siku nne wala tano. Lakini bora ni kuharakisha kufanya hivo. Bora ni mtu aharakishe kutoa rambirambi tangu pale anapokufa maiti. Lengo ni ili awafanyie wepesi wafiwa wa maiti. Lakini endapo hakuwahi kuwapa pole isipokuwa baada ya siku mbili, tatu au nne ni sawa. Hakuna kikomo cha muda uliowekwa na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/4350/ما-حكم-التعزية-بواسطة-الجراىد-والصحف
  • Imechapishwa: 17/06/2022