Ibaadhiyyah wanaposema al-Baraa´ kwa Maswahabah wanakusudia nini?


Swali: Kunamaanishwa nini kunaposemwa al-Baraa´ katika madhehebu ya Ibaadhiyyah?

Jibu: Mujtahid wa ummah, nguzo ya Ummah, Mujtahid wa ki-Ibaadhiy, mkuu, ´Allaamah Muhammad bin Yuusuf Atwfiysh katika kitabu chake kinachoitwa “adh-Dhahab al-Khaalisw”:

al-Baraa´ maana yake kilugha ni kujiweka mbali na kitu na kujitakasa nacho.  Maana yake kishari´ah ni kubughudhi, kutukana na kumlaani kafiri juu ya ukafiri wake.”[1]

Bi maana ukafiri wa shirki au ukafiri wa kukufuru neema ambao ni ufuska. Hivyo ndivyo alivyobainisha katika kitabu chake kingine kinachoitwa “Shaamil al-Aswl wal-Far´”[2].

[1] uk. 45.

[2] uk. 24.

  • Mhusika: Abuu Swaalih Mustwafaa ash-Sharqaawiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kuntu ibaadhwiyyaa yaa layta qawmiy ya´lamuun, uk. 16-17
  • Imechapishwa: 11/06/2017