Swali: Ni yapi maoni yako kwa mtu ambaye anajulikana kuwa ni walii wa Allaah. Lakini hata hivyo anavuta sigara na hawaswalishi watu Ijumaa. Lakini hata hivyo ana elimu. Elimu ni nuru ya Allaah ambayo haimpi mtenda dhambi. Vipi tutaoanisha haya?

Jibu: Ni kweli anaweza kuwa na elimu lakini ni mwanachuoni mpotevu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Kikubwa ninachokikhofia juu ya Ummah wangu ni viongozi wenye kupotosha.”

Sio kila mwanachuoni anakuwa ni mwanachuoni wa uongofu. Kuna wanachuoni wa upotevu ambapo huyu ni mmoja wao. Watu wasidanganyike nae.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Furqaan (11) http://alfawzan.af.org.sa/node/2054
  • Imechapishwa: 13/02/2017