Swali: Nikimzungumzia rafiki yangu juu ya mtu ambaye hamjui inahesabika ni katika kusengenya?

Jibu: Ndio. Ikiwa anaweza kumjua inakuwa ni katika usengenyi. Ama ikiwa hawezi kumjua… lakini lililo bora ni kusema “kuna baadhi ya watu… “ na wala usisemi “kuna mtu… “. Sema “baadhi ya watu wanafanya kadhaa” na wala usilengi. Kwa sababu ukisema “kuna mtu… “ huenda yule unayemzungumzisha akamtambua.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (03) http://audio2.islamweb.net/lecturs/aalrrajhee/430/430.mp3
  • Imechapishwa: 06/04/2018