Hukumu ya mtoto aliyezaliwa kabla ya wanandoa kufunga ndoa

Swali 08: Kuna mwanaume ni muislamu ambaye alizini na mwanamke ambaye sio muislamu na akambebea ujauzito. Baada ya kumzalia mtoto ndipo akasilimu. Ni ipi hukumu ya mtoto? Je, anazingatiwa kuwa ni mtoto wa Kishari´ah?

Jibu: Mtoto sio wa Kishari´ah. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mtoto ni wa kitandani na mzinzi anastahiki [kupigwa] mawe.”

Mtoto ni mwenye kumfuata mama yake. Mzinzi anatakiwa kutubia.

Ama kuhusu kumuoa ikitambulika kuwa alitubia baadaye basi hakuna neno. Vinginevyo basi Allaah (´Azza wa Jall) amesema:

وَحُرِّمَ ذَٰلِكَ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ

“Imeharamishwa hayo kwa waumini.”[1]

Bi maana mwanaume mwenye kujichunga na machafu kumuoa mwanamke mzinifu. Ikitambulika kuwa mwanamke ametubia kutokamana na uzinzi na akaingia ndani ya Uislamu hakuna ubaya akamuoa.

[1] 24:03

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tuhfat-ul-Mujiyb, uk. 60
  • Imechapishwa: 28/03/2020