Hukumu ya kuwapongeza makafiri wakati wa sikukuu zao

Makafiri wakioa, wakipata mtoto, amefika au amepotea mtu, wamesalimika kutokamana na chenye kuchukiza au mfano wa hayo, basi kumepokelewa mapokezi mbalimbali kutoka kwa Ahmad kama inafaa kuwapongeza kwa mambo hayo au haifai. Mara fulani anaruhusu na wakati mwingine anakataza. Kuhusiana na suala hili ni kama jambo linalohusiana na kuwapa pole kwa kufiliwa na kumtembelea mgonjwa. Hakuna tofauti kati ya mambo hayo mawili. Lakini hata hivyo mtu anatakiwa kujichunga asije kutumbukia katika yale wanayotumbukia wajinga pale wanapotamka kwa matamshi yanayofahamisha kuridhika na dini yao. Mfano wa matamshi hayo ni pale mtu anaposema:

“Allaah akufurahishe kwa dini yako”, Allaah akutie nguvu” au “Allaah akutukuze.”

Isipokuwa tu ikiwa kama mtu atasema:

“Allaah akukirimu Uislamu”, “Allaah akutukuze kwa Uislamu” na mfano wake.

Kuhusu kuwapongeza kwa nembo za kufuru ambazo ni maalum kwao kama sherehe kikafiri kama mfano wa sikukuu na funga. Kama kusema:

“Nakutakia sikukuu yenye furaha.”

Kitendo hichi, mwenye nacho akisalimika na ukafiri basi ni miongoni mwa mambo ya haramu. Ni jambo ambalo liko katika kiwango cha kuwapongeza kwa kusujudia kwake msalaba. Bali kitendo hicho [cha pongezi] ni dhambi kubwa mbele ya Allaah na cha hasira zaidi mbele Yake kuliko kumpongeza kwa kunywa pombe, kuiua nafsi, kuizini tupu ya haramu na mfano wake.

Watu wengi ambao hawajui hadhi ya dini wanatumbukia katika jambo hilo ilihali hawajui ubaya wa walichokifanya. Anayempongeza mja kwa maasi, uzushi au ukafiri basi amejipelekea mwenyewe katika hasira na ghadhabu za Allaah.

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn bin Qayyim-il-Jawziyyah (kfk. 751)
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam Ahl-idh-Dhimmah (1/441)
  • Imechapishwa: 16/12/2019