Hukumu ya kutanguliza au kuchelewesha zakaah

Swali: Je, inajuzu kuiharakisha au kuichelewesha zakaah kutokana na haja kama mfano wa kuja kwa fakiri, kutopatikana wale wenye kuiistahiki katika mji huo au sababu nyingine?

Jibu: Kuitanguliza ni jambo linafaa. Kuhusu kuichelewesha haijuzu isipokuwa ikiwa kama hapatikana mahali alipo yule mwenye kuiistahiki au akaichelewesha kutokana na haja nyingine kubwa kama kwa mfano watu wakasema kuwa katika Ramadhaan mafukara wanakuwa matajiri na hivyo akawa ameichelewesha mpaka katika Shawwaal, Dhul-Qa´daa au Dhul-Hijjah kwa sababu wakati huo ndio wanakuwa na haja kubwa. Katika hali hii ni sawa. Lakini ni juu yake kuifungamanisha na kifungu kwa sababu anaweza kufa na wajibu ulio juu yake ukapotea.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (41) http://binothaimeen.net/content/1511
  • Imechapishwa: 08/10/2018