Hukumu ya kuhudhuria swalah ya ijumaa na za mkusanyiko kwa msafiri anapofika mjini anakoenda


Swali: Baada ya msafiri kutua katika mji inajuzu kwake kuacha kwenda kuswali swalah ya ijumaa na viyo hivyo swalah za mkusanyiko?

Jibu: Hapana, haijuzu. Ni lazima kwa yule mwenye kusikia wito amuitikie mwitaji. Ni mamoja ambaye ni mkazi au msafiri. Mwenye kutua katika mji siku ya ijumaa ilihali ni msafiri na anasikia adhaana basi ni lazima kuitikia. Allaah (Ta´ala) amesema:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا نُودِيَ لِلصَّلَاةِ مِن يَوْمِ الْجُمُعَةِ فَاسْعَوْا إِلَىٰ ذِكْرِ اللَّـهِ

“Enyi walioamini! Kunaponadiwa kwa ajili ya swalah siku ya ijumaa, basi kimbilieni katika Dhikr ya Allaah.” (62:09)

Tunamuuliza msafiri huyu: je, wewe ni katika waumini au hapana? Atasema: ni katika waumini. Basi ukiwa wewe ni katika waumini ni lipi jibu lako kwa Allaah siku ya Qiyaamah ilihali ameelekeza uzungumzishwaji Kwako na akasema:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا نُودِيَ لِلصَّلَاةِ مِن يَوْمِ الْجُمُعَةِ فَاسْعَوْا إِلَىٰ ذِكْرِ اللَّـهِ

“Enyi walioamini! Kunaponadiwa kwa ajili ya swalah siku ya ijumaa, basi kimbilieni katika Dhikr ya Allaah.”?

Tukikadiria kuwa mtu yuko njiani anasafiri na akapita katika mji na huku akamsikia muadhini, katika hali hii tunasema kuwa si lazima kwake kubaki na kuswali. Kwa sababu bado uko njiani unasafiri. Lakini mtu ambaye ni mkazi amekwishatua ni lazima kwake kuhudhuria. Vivyo hivyo ndio yanayosemwa juu ya swalah ya mkusanyiko. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema kuhusu swalah ya mkusanyiko:

“Mwenye kusikia wito na asiitikie, basi hana swalah isipokuwa akiwa na udhuru.”

Safari sio udhuru. Kwa dalili kwamba Allaah ameamrisha kuswali swalah kwa mkusanyiko katika hali ya vita.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa' ash-Shahriy (69) http://binothaimeen.net/content/1550
  • Imechapishwa: 28/06/2019