Swali: Ni ipi hukumu ya mwenye kutawadha na akaosha mkono wa kushoto kabla ya wa kulia?
Jibu: Hakuna neno. Lakini ni jambo linaenda kinyume na Sunnah. Sunnah ni kuanza kwa upande wa kulia kama tulivyopitia katika Hadiyth. Sunnah ni yeye kuanza kwa upande wa kulia.
- Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (35) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo--1431-11-09.mp3
- Imechapishwa: 15/11/2014