Hivi ndivo unatakiwa kudhihirisha Uislamu katika mji wa kikafiri

Swali: Ni yepi maelezo kuhusu kudhihirisha dini katika miji ya kikafiri kuhusiana na muisamu anayeishi katika nchi kama hiyo?

Jibu: Ina maana kwamba alinganie katika dini ya Allaah na wala asinyamaze. Analingania katika dini ya Allaah, analingania katika Uislamu, anasimamisha dini yake na wala haachi chochote katika dini. Anaswali, anafunga na anafanya mambo yote ya dini yake. Haachi chochote katika dini yake kwa sababu ya kuwaridhisha makafiri au ili aweze kuishi nao. Haachi chochote katika dini yake. Huku ndio kudhihirisha dini. Kudhihirisha dini hakuna maana kwamba wanakuacha ukaswali, ukafunga na wala hawakufanya lolote. Huku sio kudhihirisha dini. Kudhihirisha dini ni kuwabainishia yale waliyomo katika kufuru na uwalinganie kwa Allaah (´Azza wa Jall). Ionyeshe dini yako na wala usijifiche. Wapo baadhi ya waislamu huko ambao wanajificha wanaposwali. Wanaswali sehemu zilizojificha na wala hawaidhihirishi dini yao kwa sababu wanawaogopa makafiri. Hii ni khasara. Idhihirishe dini yako. Dini yako ni utukufu. Wao wanapomuona mtu ameshikamana barabara na dini yake wanamuheshimu zaidi tofauti na yule wanayemuona anaichukulia wepesi dini yake ambapo wanamtawala. Allaah anawaacha wakamtawala. Dini ni utukufu na sio kitu ambacho kinatakiwa kufichwa kutokamana na watu. Bali inatakiwa kuonyeshwa. Wapo wengi ambao wanasilimu kwa sababu ya kuwaona waislamu wanaswali na kutoa adhaana. Matokeo yake Uislamu unaingia katika nyoyo zao.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (88)
  • Imechapishwa: 07/09/2018