Nilimsikia Abu ´Abdillaah akiulizwa kuhusu mwanamme ambaye anatoa fatwa pasi na elimu. Akajibu:

“Imepokelewa kwamba Abu Muusa (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

“Anajipenyeza kupitia dini yake.”[1]

Abu ´Abdillaah amesema:

“Hivi kweli inawezekanaje mtu ambaye anatambua Sunnah kutoka kwa Mtume wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) lakini hata hivyo akachagua kutoa fatwa inayokwenda kinyume?”

Alionekana amelichukulia khatari jambo hilo.

[1] ad-Daarimiy (1/274).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Abiy Harb al-Jarjaara’iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Masaa-il-ul-Imaam Ahmad, uk. 99
  • Imechapishwa: 28/03/2021