Swali: Allaah (Ta´ala) amesema:

لَا يَسْتَأْذِنُكَ الَّذِينَ يُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ أَن يُجَاهِدُوا بِأَمْوَالِهِمْ وَأَنفُسِهِمْ ۗ وَاللَّـهُ عَلِيمٌ بِالْمُتَّقِينَ

“Hawakuombi ruhusa [ya kubakia nyuma] wale waliomwamini Allaah na Siku ya Mwisho wasifanye jihaad kwa mali zao na nafsi zao. Na Allaah ni Mjuzi kwa wenye taqwa.” (09:44)

Kuna ambao wanatumia Aayah hii kama dalili juu ya kujuzu kutoka kwenda katika Jihaad bila ya idhini ya kiongozi. Ni ipi maana ya Aayah hii? Je, dalili hii…

Jibu: Ametakasika Allaah! Allaah amesema:

لَا يَسْتَأْذِنُكَ

“Hawakuombi ruhusa [ya kubakia nyuma]… ”

Ni nani mwenye kuombwa idhini? Ni nani ambaye Allaah (Jalla wa ´Alaa) anamzungumzisha? Ni dalili yenye kuonesha kuwa mtawala ndiye mwenye kutoa idhini ya Jihaad au kutoitoa. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ndiye ambaye alikuwa mtawala. Leo hii viongozi baada yake. Tazama dalili hii iliyopinda! Wanatumia hoja kwa dalili ilio dhidi yao:

لَا يَسْتَأْذِنُكَ

“Hawakuombi ruhusa [ya kubakia nyuma] wale… ”

Ni dalili yenye kuonesha kuwa yule mwenye kutakwa idhini juu ya Jihaad au kutokuwepo Jihaad kwa sababu ya udhuru ilikuwa ni Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Yeye ndiye aliyekuwa kiongozi. Vivyo hivyo wale watawala wa waislamu waliokuja baada yake.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Tafsiyr-ish-Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (23) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tafsirayat-12-07-1435-01_0.mp3
  • Imechapishwa: 18/05/2018