Imaam Ibn-ul-Qayyim (Rahimahu Allaah) amesema:

“Kipambanuzi kinachopambanua kushikamana na njia ilionyooka na kupondoka nayo ni ile njia ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Maswahabah zake.”[1]

Hiki ndio kipambanuzi. Kwa sababu kila mmoja anadai kuwa yuko katika haki na kwamba njia yake ndio ya sawa na kwamba wengine wote wamepotea. Kipambanuzi kinachopambanua njia ilionyooka ni ile njia ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Maswahabah zake. Hii ndio njia ilionyooka – na sio yale waliyomo wapotevu, wajinga na wale watu wanaojidai elimu.

[1] Ighaathat-ul-Lahfaan (1/96).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (34) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/ighastah%20-%201%20-%202%20-%201436.mp3
  • Imechapishwa: 04/06/2020