Swali: Kuna sababu ipi ya nyama ya ngamia kuchengua wudhuu´?

Jibu: Allaah ndiye mjuzi zaidi. Allaah (Jall wa ´Alaa) ndiye anajua zaidi. Yeye ni Mwenye kurehemu, Mwingi wa hekima. Haamrishi isipokuwa kwa kitu kilicho na hekima na wala hakatazi isipokuwa kwa kitu kilicho na hekima (Subhaanah):

إِنَّ رَبَّكَ حَكِيمٌ عَلِيمٌ

”Hakika Mola wako ni Mwingi wa hekima, Mjuzi wa yote.”[1]

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Tawadheni kwa nyama ya ngamia na wala msitawadhe kwa nyama ya kondoo.”

Haya yalisemwa na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wakati alipoulizwa:

”Tutawadhe kwa nyama ya ngamia?”

Akajibu:

”Ndio.”

Wakauliza tena:

”Tutawadhe kwa nyama ya kondoo?”

Akasema:

”Ukitaka.”

Tumetosheka kwamba Mtume ametuamrisha kutawadha. Haya yanatutosha. Kuhusu hekima Allaah ndiye mjuzi zaidi.

[1] 06:83

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa ad-Duruus https://binbaz.org.sa/fatwas/3768/%D9%85%D8%A7-%D8%A7%D9%84%D8%B9%D9%84%D8%A9-%D9%81%D9%8A-%D9%86%D9%82%D8%B6-%D9%84%D8%AD%D9%85-%D8%A7%D9%84%D8%A7%D8%A8%D9%84-%D8%A7%D9%84%D9%88%D8%B6%D9%88%D8%A1
  • Imechapishwa: 06/03/2020