Swali: Ni ipi Radd kwa mwenye kusema “tunaweka wakati na kati kwa kuwa ni wenye madhambi”?

Jibu: Haya ndio maneno ya washirikina wa mwanzoni. Walikuwa wanasema kuwa wanawafanya kuwa ni waombezi wao mbele ya Allaah kwa kuwa ni wenye madhambi na wao watawaombea mbele ya Allaah. Allaah akawaraddi kwa hilo na kuonelea kuwa ni shirki:

وَيَعْبُدُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ مَا لَا يَضُرُّهُمْ وَلَا يَنفَعُهُمْ وَيَقُولُونَ هَـٰؤُلَاءِ شُفَعَاؤُنَا عِندَ اللَّـهِ

“Na wanaabudu asiyekuwa Allaah ambao [hawawezi] kuwadhuru na wala kuwanufaisha na wanasema: “Hawa ni waombezi wetu mbele ya Allaah.” (10:18)

Amesema kuwa wanawaabudu:

وَيَعْبُدُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ

“Na wanaabudu asiyekuwa Allaah…”

Hawasemi kuwa ni washirika wetu, bali wanasema kuwa “ni waombezi wetu”. Shirki ni shirki hata kama itaitwa kwa jina lingine. Haijalishi kitu hata kama itaitwa kuwa ni uombezi, ni shirki. Haijuzu. Maneno hayabadilishi uhakika.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo–1430-4-23.mp3
  • Imechapishwa: 09/11/2014