Mtu ambaye anajinasibisha na makundi ya leo kama mfano wa Jamaa´at-ut-Tabliygh, al-Ikhwaan al-Muslimuun, Hizb-ut-Tahriyr au Jamaa´at-ut-Takfiyr wal-Hijrah anajenga mapenzi na chuki yake kwa ajili ya kundi lake. Haijuzu kusema kuwa huyu ni katika Ahl-us-Sunnah katika suala hili. Mwenye kusema kuwa ni katika Ahl-us-Sunnah pasi na kufungamanisha na akanyamaza amekosea. Midhali mtu huyu anapenda na kuchukia kwa ajili ya kundi hili au anajinasibisha na kundi hili au anaridhia kujinasibisha na kundi amejichafua kwa Bid´ah hii mbaya amewafarikisha waislamu na amesababisha uadui na chuki kati yao. Ikiwa mtu huyu kweli anaenda sambamba na Sunnah katika mambo yote isipokuwa suala hili tu basi ni lazima kusema kuwa sio Ahl-us-Sunnah katika suala hili. Kwa sababu msimamo wa Sunnah juu ya ukundi-ukundi kama huu unajulikana, uko wazi na bayana.

Kuna mtu alikuja kwa Imaam Maalik na kumwambia:

“Ee Abu ´Abdillaah! Nataka kukuuliza juu ya jambo ambalo nitalitumia kama hoja kati yangu mimi na Allaah (´Azza wa Jalla).” Imaam Maalik akasema: “Uliza.” Akasema: “Ni kina nani Ahl-us-Sunnah?” Akajibu: “Ahl-us-Sunnah ni wale wasiokuwa na jina wanalotambulika nalo; si Jahmiy, si Qadariy, wala Raafidhwiy… “[1]

[1] al-Intiqaa’ (35) ya Ibn ´Abdil-Barr.

  • Mhusika: Shaykh ´Abdus-Salaam bin Barjas Aal ´Abdil-Kariym
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Jarh wat-Ta´diyl ´indas-Salaf, uk. 42-44
  • Imechapishwa: 09/08/2020