Qadariyyah wamepinga Qadar kwa utata wa kwamba wamesema hivo ili hilo lisilazimishe Akawa ameumba maasi na Yeye huyo huyo ndio akawa mwenye kuyaadhibu. Hilo ni kutokana na kwamba wamejenga juu ya asli ambayo: ni wajibu kwa Allaah kumfanyia mja mambo yaliyo mema. Matendo ambayo ni mema kwa mja ni Yeye kumkadiria utiifu na si maasi. Lau atakadiria maasi na akaadhibu kwayo, basi hilo litamlazimikia [awe] ameyaumba maasi na awe mwenye kuadhibu kwayo.

Radd kwao tunawaambia kuwa wamekimbia kitu na wakatumbukia kwenye kitu kiovu zaidi kuliko walichokikimbia. Maneno yao yanalazimisha matakwa ya kafiri ni yenye kushinda matakwa ya Allaah. Kwa mujibu wa maneno yao ni kwamba Allaah amemtakia kafiri huyu imani lakini kafiri huyu yeye akawa amejitakia kufuru. Hivyo matakwa ya kafiri huyu yakawa yametokea na matakwa ya Allaah yakawa hayakutokea! Hii ni I´tiqaad ilio mbaya kabisa na ni maneno yasokuwa na dalili yoyote. Isitoshe maneno haya yanakwenda kinyume na dalili ya andiko na akili. Hivi kweli kuna mpotevu kuliko mwenye kusema kuwa Allaah amemtakia kafiri imani lakini kafiri huyo akawa amejitakia mwenyewe kufuru? Ina maana matakwa ya kafiri yameshinda matakwa ya Allaah?

Pili ni kwamba maneno yao yanalazimisha kutokee katika ufalme wa Allaah yale asiyoyataka.

Tatu maneno yao yanalazimisha kushirikisha katika uola na kuwa Allaah sio Muumba wa matendo ya wanyama na ya waja. Madhehebu ya Qadariyyah hawa ni kwamba Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) juu ya kila kitu sio Muweza, waja wanawezeshwa katika mambo wasiyoyaweza, Allaah (Subhaanah) hawezi kumwongoza mpotevu wala kumpotosha mwongofu. Wanachuoni wamesema juu ya haya kwa kifupi kuwa ni kumshirikisha Allaah katika uola. Kwa ajili hii ndio maana Qadariyyah wakaitwa kuwa ni waabudu moto, Majuus, wa Ummah huu na kwamba maneno yao yanafanana na maneno ya wenye kuabudu moto.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajhiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Hidaayah ar-Rabbaaniyyah fiy Sharh al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah (01/357-358)
  • Imechapishwa: 21/05/2020