Hapa ndipo sunnah ya Fajr inaweza kuswaliwa baada ya fajr

Swali: Kipindi ambapo naswali Raatibah ya Fajr kunakimiwa swalah; niikamilishe au niikatishe?

Jibu: Ikiwa uko mwishoni ikamilishe na ikiwa ndio waanza ikatishe.

Swali: Nikiikata, niiswali moja kwa moja baada ya swalah ya faradhi?

Jibu: Ndio. Iswali moja kwa moja baada ya Fajr au baada ya jua kuchomoza.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Fath-il-Majiyd (26) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/fathul%20%20-%204%20-%201%20-%201436.mp3
  • Imechapishwa: 11/02/2017