Hapa ndipo mazoezi ya wanawake yatajuzu

Swali: Katika mji wetu wanawake wanakusanyika katika nyukumbi za mazoezi na wanacheza dufu na ngoma kwa lengo la mazoezi. Je, kitendo kama hichi kinajuzu?

Jibu: Mazoezi ambayo yana manufaa kwa mwili yanajuzu kwa sharti ikiwa wanawake wamejisitiri na hakuna wanaume wanaowaona. Katika hali hii mazoezi ni sawa. Lakini ikiwa yanaambatana na dufu na nyimbo, ni haramu. Kwa kuwa ni katika upuuzi wa haramu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (01) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/omdh–14340126_0.mp3
  • Imechapishwa: 25/08/2020