Hapa ndipo matembezi yatamfaa mtu

Swali: Ni upi usahihi wa Hadiyth:

“Mwenye kunitembelea basi uombezi wangu umewajibika kwake”?

Jibu: Hadiyth hii ni dhaifu sana na imezuliwa. Si Swahiyh. Uombezi wa Mtuem (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) unapatikana kwa Tawhiyd na imani. Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) alisema hali ya kumuuliza:

“Ni nani mwenye furaha zaidi ya uombezi wako, ee Mtume wa Allaah?” Akasema: “Yule atakayesema ´hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah` hali ya kuwa ni mtakasifu kutoka moyoni mwake.”

Jambo hili ni jepesi zaidi kuliko matembezi.

Kuhusu yule mwenye kutembelea kaburi lake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ilihali matendo yake ni maovu, ni mshirikina au ni mwenye kuendelea juu ya maasi au Bid´ah, hakika hayatomfaa kitu matembezi haya. Ama akimtembelea na huku ni mwenye kumpwekesha Allaah  basi matembezi hayo yatamfaa.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (12) https://audio.islamweb.net/audio/index.php?page=audioinfo&audioid=191546
  • Imechapishwa: 29/09/2019