Hapa ndipo atakufurishwa mganga


Swali: Je, mganga anatakiwa kukufurishwa pasi na kumsimamishia hoja?

Jibu: Ni jambo la lazima. Hakufurishwi yeyote isipokuwa baada ya kumsimamishia hoja. Kwa sababu pengine akawa mjinga na hajui. Au amewaona watu wakifanya jambo hilo na yeye akafikiria kuwa ni jambo linalofaa. Kwa hivyo ni lazima:

وَمَا كُنَّا مُعَذِّبِينَ حَتَّىٰ نَبْعَثَ رَسُولًا

”Hatukuwa Wenye kuadhibu mpaka tumtume Mtume.” (17:15)

Kwa hivyo anatakiwa kusimamishiwa hoja.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Fath-il-Majiyd (63) http://alfawzan.af.org.sa/ar/node/16641
  • Imechapishwa: 12/03/2021