Swali: Mimi ni mwalimu na wakati mwingine nalazimika kusambaza maswali na kuwachunga wanafunzi. Nina hali mbalimbali:

Ya kwanza: Niikimwambia mwanafunzi maalum kwamba arudi kutatua swali. Je, huku kunahesabika ni kughushi?

 Ya pili: Nikimwambia mwalimu atazame tena jibu alilojibu kama ni sahihi. Lengo nataka kumzindua ili alitatue swali kwa sababu amekosea.

Ya tatu: Nikiweka maneno yakawa yenye kuenea kwa wanafunzi wote pasi na kulenga. Ni ipi hukumu ya hali zote hizi tatu?

Jibu: Yote haya ni ghushi. Ni mamoja ukiwaambia watazame jibu walilojibu au swali waliloulizwa kwa ujumla au kwa kulenga. Isipokuwa ikiwa kama swali haliko wazi. Katika hali hii ni wajibu kuwabainishia wanafunzi. Ama swali likiwa wazi, basi kuashiria jibu kunahesabika ni ghushi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (55) http://binothaimeen.net/content/1267
  • Imechapishwa: 06/10/2019