Hali ya hewa -40 wakati wa Fajr


Swali: Katika nchi yetu hali ya hewa ni -40 wakati wa swalah ya Fajr. Katika hali hii inajuzu kuswali nyumbani na mtu asiswali na mkusanyiko?

Jibu: Ndio. Ikiwa inaathiri afya yake, aswali huko nyumbani. Ikiwa haiathiri afya yake na anaweza kuvaa mavazi ya joto, aswali na mkusanyiko.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Fath-il-Majiyd (55) http://alfawzan.af.org.sa/ar/node/16503
  • Imechapishwa: 23/09/2017